Hosea 10:11-12
11 aEfraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwaambaye hupenda kupura,
hivyo nitamfunga nira
juu ya shingo yake nzuri.
Nitamwendesha Efraimu,
Yuda lazima alime,
naye Yakobo lazima avunjavunje
mabonge ya udongo.
12 bJipandieni wenyewe haki,
vuneni matunda ya upendo usio na kikomo,
vunjeni ardhi yenu isiyolimwa;
kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana,
mpaka atakapokuja
na kuwanyeshea juu yenu haki.
Copyright information for
SwhNEN