‏ Hebrews 9:18-22

18 aHii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 19 bMose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 20 cAlisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 21 dVivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada. 22 eKwa kweli sheria hudai kwamba, karibu kila kitu kitakaswe kwa damu, wala pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.

Copyright information for SwhNEN