Hebrews 7:17-22
17 aKwa maana imeshuhudiwa kwamba:“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
18 bKwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa 19 c(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.
20Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 21 dlakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia:
“Bwana ameapa
naye hatabadilisha mawazo yake:
‘Wewe ni kuhani milele.’ ”
22 eKwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Copyright information for
SwhNEN