‏ Habakkuk 2:6-11

6 a“Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema,

“ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa
na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu!
Ataendelea hivi kwa muda gani?’
7 bJe, wadai wako hawatainuka ghafula?
Je, hawataamka na kukufanya utetemeke?
Kisha utakuwa mhanga kwao.
8 c dKwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi,
watu waliobaki watakuteka nyara wewe.
Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu;
umeharibu nchi na miji, na kila mmoja ndani yake.

9 e“Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu,
awekaye kiota chake juu,
ili kukimbia makucha ya uharibifu!
10 fUmefanya shauri la maangamizi ya watu wengi,
ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako.
11 gMawe ya kuta yatapiga kelele,
na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.