Genesis 6:11-13
11 aWakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. 12 bMungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 13 cKwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.
Copyright information for
SwhNEN