‏ Genesis 50:10-12

10 aWalipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. 11 bWakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.
Abel-Mizraimu maana yake Maombolezo ya Wamisri.


12Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza:
Copyright information for SwhNEN