Genesis 34:2-6
2 aIkawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi. 3Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. 4 bShekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.”5 cYakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.
6 dKisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo.
Copyright information for
SwhNEN