‏ Genesis 31:44-52

44 aNjoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.”

45 bHivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. 46 cAkawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. 47 dLabani akaliita Yegar-Sahadutha
Yegar-Sahadutha maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiaramu.
na Yakobo akaliita Galeedi.
Galeedi maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiebrania.


48 gLabani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. 49 hPia liliitwa Mispa,
Mispa maana yake Mnara wa ulinzi.
kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.
50 jKama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

51 kPia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi. 52 lLundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru.
Copyright information for SwhNEN