‏ Genesis 30:3-10

3 aNdipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”

4 bHivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili, 5Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana. 6 cNdipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.
Dani maana yake Anahukumu, yaani Mungu amenipa haki yangu.


7Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 8 eNdipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.
Naftali maana yake Nimeshindana nami nimeshinda.


9 gLea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake. 10Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana.
Copyright information for SwhNEN