‏ Genesis 25:12-16

Wana Wa Ishmaeli

12 aHivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu.

13 bHaya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 14 cMishma, Duma, Masa, 15 dHadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. 16 eHawa walikuwa wana wa Ishmaeli na haya ni majina ya viongozi wa makabila kumi na mawili kulingana na makao yao na kambi zao.
Copyright information for SwhNEN