Genesis 2:21-23
21 aHivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 22 bKisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.23 cHuyo mwanaume akasema,
“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke,’ ▼
▼Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume.
kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”
Copyright information for
SwhNEN