Genesis 11:25-29
25Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.26 aTera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani.
Wazao Wa Tera
27 bHawa ndio wazao wa Tera.Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. 28 cTera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. 29 dAbramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani.
Copyright information for
SwhNEN