‏ Genesis 10:14-19

14 aWapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15 bKanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,
16 cWayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17 dWahivi, Waariki, Wasini, 18 eWaarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,
19 fna mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

Copyright information for SwhNEN