Galatians 5:16-24
Maisha Ya Kiroho
16 aKwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 bKwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. 18 cLakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.19 dBasi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 ehusuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
22 fLakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. 24Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake.
Copyright information for
SwhNEN