‏ Ezra 8:24-30

24Kisha niliwatenga viongozi wa makuhani kumi na wawili, pamoja na Sherebia, Hashabia na ndugu zao kumi, 25 anami nikawapimia fedha, dhahabu na vifaa ambavyo mfalme, washauri wake, maafisa wake na Israeli wote waliokuwepo walikuwa wamevitoa sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. 26Niliwapimia talanta 650
Talanta 650 za fedha ni sawa na tani 25.
za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,
Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.
talanta mia moja za dhahabu,
27mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja,
Darkoni 1,000 ni sawa na kilo 8.5.
na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu.

28 eNiliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu. 29 fVilindeni kwa uangalifu mpaka mtakapovipima ndani ya vyumba vya nyumba ya Bwana katika Yerusalemu mbele ya makuhani, viongozi na Walawi pamoja na wakuu wa jamaa za Israeli.” 30Ndipo makuhani na Walawi wakapokea fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu ambavyo vilipimwa na kupelekwa katika nyumba ya Mungu wetu mjini Yerusalemu.

Copyright information for SwhNEN