Ezekiel 48:15-18
15 a“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,000 ▼▼Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25.
na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 16 cnao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500, ▼▼Dhiraa 4,500 ni sawa na kilomita 2.025.
upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. 17Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 250 ▼▼Dhiraa 250 ni sawa na sentimita 112.5.
upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi. 18 fEneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.
Copyright information for
SwhNEN