Ezekiel 45:1-8
Mgawanyo Wa Nchi
1 a“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000, ▼▼Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25.
upana wake dhiraa 20,000 ▼▼Dhiraa 20,000 ni sawa na kilomita 9.
eneo hili lote litakuwa takatifu. 2 dKatika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. 3 eKatika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. ▼▼Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5.
Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu. 4 gItakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu. 5 hEneo la urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000 litakuwa la Walawi wale wanaotumika hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi. 6 i“ ‘Utatoa mji kama mali yao wenye upana wa dhiraa 5,000 ▼
▼Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25.
na urefu wa dhiraa 25,000, karibu na sehemu takatifu, itakuwa mali ya nyumba yote ya Israeli. 7 k“ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na lile eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu upande huu na upande huu na eneo la mji. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi na upande wa mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila. 8 lNchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.
Copyright information for
SwhNEN