Ezekiel 37:26-28
26 aNitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele. 27 bMaskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 28 cNdipo mataifa watakapojua kwamba Mimi Bwana ndiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”
Copyright information for
SwhNEN