‏ Ezekiel 30:13-19

13 a“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu
na kukomesha vinyago katika Memfisi
Kiebrania ni Nofu.

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,
nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
14 cNitaifanya Pathrosi
Pathrosi ni Misri ya Juu.
kuwa ukiwa
na kuitia moto Soani,
nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi
Thebesi kwa Kiebrania ni No (au No-Amoni), mji katika Misri.

15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,
Kiebrania ni Sini.

ngome ya Misri,
nami nitakatilia mbali
makundi ya wajeuri wa Thebesi.
16 gNitaitia moto nchi ya Misri;
Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.
Thebesi itachukuliwa na tufani,
Memfisi itakuwa katika taabu daima.
17 hWanaume vijana wa Oni
Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).
na wa Pi-Besethi
Yaani Bubasti.

wataanguka kwa upanga
nayo hiyo miji itatekwa.
18 kHuko Tahpanhesi mchana utatiwa giza
nitakapovunja kongwa la Misri;
hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.
Atafunikwa na mawingu
na vijiji vyake vitatekwa.
19 lKwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,
nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”
Copyright information for SwhNEN