‏ Ezekiel 19:9-14

9 aKwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu
na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli.
Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake
hakukusikika tena
katika milima ya Israeli.

10 b“ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu
katika shamba lako la mizabibu
uliopandwa kando ya maji,
ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi
kwa sababu ya wingi wa maji.
11 cMatawi yake yalikuwa na nguvu,
yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.
Ulikuwa mrefu kupita miti mingine
katikati ya matawi manene;
ulionekana kwa urahisi
kwa ajili ya urefu wake
na wingi wa matawi yake.
12 dLakini ulingʼolewa kwa hasira kali
na kutupwa chini.
Upepo wa mashariki uliufanya usinyae,
matunda yake yakapukutika,
matawi yake yenye nguvu yakanyauka
na moto ukayateketeza.
13 eSasa umepandwa jangwani
katika nchi kame na ya kiu.
14 fMoto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwa
na kuteketeza matunda yake.
Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake
lifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’
Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”

Copyright information for SwhNEN