‏ Exodus 37:25-28

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

(Kutoka 30:1-5)

25 aAkatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. 26Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. 27Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko iliyotumika kuyabebea madhabahu. 28 bAkatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.

Copyright information for SwhNEN