‏ Exodus 30:11-16

Fedha Ya Upatanisho

11Naye Bwana akamwambia Mose, 12 a“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 13 bKila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,
Nusu shekeli ni sawa na gramu 6.
kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.
Gera 20 ni sawa na shekeli moja au gramu 12.
Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana.
14 eWote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana. 15 fMatajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. 16 gUtapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”

Copyright information for SwhNEN