‏ Exodus 29:4-9

4 aKisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 5 bChukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. 6 cWeka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. 7 dChukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. 8 eWalete wanawe na uwavike makoti, 9 fpia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe.


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.