Exodus 28:39-43
39 a“Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. 40 bWatengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. 41 cBaada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.42 d“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. 43 eAroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa.
“Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.
Copyright information for
SwhNEN