Exodus 27:10-18
10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini, ▼
▼Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. 13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano ▼▼Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.
kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16 c“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini ▼
▼Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.
la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. 17Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. 18Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba.
Copyright information for
SwhNEN