‏ Exodus 24:15-18

15 aMose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 16 bnao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu. 17 cKwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 18 dKisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.