‏ Exodus 23:14-19

Sikukuu Tatu Za Mwaka

(Kutoka 34:18-26; Kumbukumbu 16:1-17)

14 a“Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu.

15 b“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri.

“Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.

16 c“Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako.

“Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani.

17“Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi.

18 d“Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu.

“Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi.

19“Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Copyright information for SwhNEN