‏ Exodus 22:25-27

25 a“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. 26 bKama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, 27 ckwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

Copyright information for SwhNEN