‏ Exodus 12:43-49

Masharti Kwa Ajili Ya Pasaka

43 a Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka:

“Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.
44 bMtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri, 45 clakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.

46 d“Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote. 47Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.

48 e“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila. 49 fSheria iyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.