‏ Ephesians 6:5-8

Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana

5 aNinyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo. 6 bWatiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 cTumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu. 8 dMkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.

Copyright information for SwhNEN