‏ Ephesians 6:10-18

Silaha Za Mungu

10 aHatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 bVaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 12 cKwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 dKwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 14 eKwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 fnayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 16 gZaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 hVaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. 18 iMkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.


Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.