Ephesians 4:7-10
7 aLakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo. 8 bKwa hiyo husema:“Alipopaa juu zaidi, ▼
▼Juu zaidi hapa ina maana mbingu za mbingu.
aliteka mateka,
akawapa wanadamu vipawa.”
9 d(Asemapo “alipaa juu,” maana yake nini isipokuwa ni kusema pia kwamba Kristo alishuka pande za chini sana za dunia? ▼
▼Pande za chini sana za dunia hapa maana yake Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu.
10 fYeye aliyeshuka ndiye alipaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.)
Copyright information for
SwhNEN