‏ Ecclesiastes 9:13-18

Hekima Ni Bora Kuliko Upumbavu

13 aPia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana: 14Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 15 bKatika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini. 16 cKwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.

17 dManeno ya utulivu ya mwenye hekima
husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa wapumbavu.
18 eHekima ni bora kuliko silaha za vita,
lakini mwenye dhambi mmoja
huharibu mema mengi.
Copyright information for SwhNEN