‏ Ecclesiastes 9:11-12

11 aNimeona kitu kingine tena chini ya jua:

Si wenye mbio washindao mashindano
au wenye nguvu washindao vita,
wala si wenye hekima wapatao chakula
au wenye akili nyingi wapatao mali,
wala wenye elimu wapatao upendeleo,
lakini fursa huwapata wote.
12 bZaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ajuaye wakati saa yake itakapokuja:

Kama vile samaki wavuliwavyo katika wavu mkatili,
au ndege wanaswavyo kwenye mtego,
vivyo hivyo wanadamu hunaswa na nyakati mbaya
zinazowaangukia bila kutazamia.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.