Deuteronomy 6:14-21
14Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; 15 akwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi. 16 bUsimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa. 17 cUtayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa. 18 dFanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako, 19 ekuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema.20 fSiku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?” 21 gMwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.
Copyright information for
SwhNEN