Deuteronomy 33:13-17
13 aKuhusu Yosefu akasema:“Bwana na aibariki nchi yake
kwa umande wa thamani
kutoka mbinguni juu,
na vilindi vya maji
vilivyotulia chini;
14pamoja na vitu vilivyo bora sana
viletwavyo na jua,
na vitu vizuri sana vinavyoweza
kutolewa na mwezi;
15 bpamoja na zawadi bora sana
za milima ya zamani
na kwa wingi wa baraka
za vilima vya milele;
16 cpamoja na baraka nzuri mno
za ardhi na ukamilifu wake,
na upendeleo wake yeye
aliyeishi kwenye kichaka
kilichokuwa kinawaka moto.
Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la uso la aliye mkuu
miongoni mwa ndugu zake.
17 dKatika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza;
pembe zake ni pembe za nyati,
na kwa pembe hizo atapiga mataifa,
hata yaliyo miisho ya dunia.
Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu;
hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”
Copyright information for
SwhNEN