‏ Deuteronomy 32:13-14


13 aAkamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,
akamlisha kwa mavuno ya mashamba.
Akamlea kwa asali toka mwambani,
na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu,
14 bkwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ngʼombe
na kutoka makundi ya mbuzi,
kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,
kwa kondoo dume wazuri wa Bashani,
na kwa ngano nzuri.
Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu.
Copyright information for SwhNEN