‏ Deuteronomy 30:12-15

12 aHakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” 13 bWala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” 14 cLa hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

15 dTazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo.
Copyright information for SwhNEN