Deuteronomy 28:21-28
21 aBwana atakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka nchi unayoingia kuimiliki. 22 bBwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.23 cAnga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma. 24 dBwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.
25 e Bwana atakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia. 26 fMizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza. 27 gBwana atakupiga kwa majipu ya Misri na kwa vidonda vitokavyo usaha na kuwashwa, ambako huwezi kuponywa. 28Bwana atakupiga kwa wazimu, upofu na kuchanganyikiwa kwa akili.
Copyright information for
SwhNEN