Amos 5:6-14
6 aMtafuteni Bwana mpate kuishi,au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto;
utawateketeza, nayo Betheli
haitakuwa na yeyote wa kuuzima.
7 bNinyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu
na kuiangusha haki chini
8 c(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni,
ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko
na mchana kuwa usiku,
ambaye huyaita maji ya bahari
na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:
Bwana ndilo jina lake;
9yeye hufanya maangamizo kwenye ngome
na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa),
10 dmnamchukia yule akemeaye mahakamani,
na kumdharau yule ambaye husema kweli.
11 eMnamgandamiza maskini
na kumlazimisha awape nafaka.
Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,
hamtaishi ndani yake;
ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,
hamtakunywa divai yake.
12 fKwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu.
Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa
na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
13Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo,
kwa kuwa nyakati ni mbaya.
14 gTafuteni mema, wala si mabaya,
ili mpate kuishi.
Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,
kama msemavyo yupo nanyi.
Copyright information for
SwhNEN