‏ Acts 2:25-28

25 aKwa maana Daudi asema kumhusu yeye:

“ ‘Nalimwona Bwana mbele yangu daima.
Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.
26Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,
na ulimi wangu unashangilia;
mwili wangu nao utapumzika kwa tumaini.
27 bKwa maana hutaniacha kaburini,
wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.
28 cUmenionyesha njia za uzima,
utanijaza na furaha mbele zako.’
Copyright information for SwhNEN