‏ 2 Samuel 5:6-7

Daudi Ateka Yerusalemu

6 aMfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.” 7 bHata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

Copyright information for SwhNEN