‏ 2 Kings 20:2-5

2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 3 a“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

4Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Bwana likamjia, akaambiwa: 5 b“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekalu la Bwana.
Copyright information for SwhNEN