2 Corinthians 9:6-9
Kupanda Kwa Ukarimu
6 aKumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. 7 bKila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. 8 cNaye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. 9 dKama ilivyoandikwa:“Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu
akawapa maskini;
haki yake hudumu milele.”
Copyright information for
SwhNEN