‏ 2 Corinthians 6:14-16

Msifungiwe Nira Pamoja Na Wasioamini

14 aMsifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 bKuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari?
Beliari hapa ina maana ya uovu, kutokumcha Mungu.
Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?
16 dKuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Copyright information for SwhNEN