‏ 2 Chronicles 36:22-23

Koreshi Atangaza Uhuru Kwa Waliokuwa Uhamishoni

(Ezra 1:1-4)

22 aKatika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Bwana lililosemwa na nabii Yeremia, Bwana aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:

23“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Yeyote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha huyo mtu na apande.’ ”

Copyright information for SwhNEN