‏ 2 Chronicles 20:31-37

Mwisho Wa Utawala Wa Yehoshafati

(1 Wafalme 22:41-50)

31 aHivyo Yehoshafati akatawala Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi. 32Alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakwenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana. 33 bHata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, na watu wakawa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa baba zao.

34 cMatukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Yehu mwana wa Hanani, ambazo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

35 dHatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya urafiki na Ahazia mfalme wa Israeli ambaye alifanya maovu sana. 36 eAkaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi,
Au: za biashara (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; Isa 2:16; 60:9).
nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi.
37 gNdipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, Bwana ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kungʼoa nanga ili kwenda Tarshishi.

‏ 2 Chronicles 21:1

Yehoramu Atawala

(2 Wafalme 8:17-24)

1 hYehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.
Copyright information for SwhNEN