‏ 1 Samuel 27:6-8

6 aHivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi mji wa Siklagi, nao Siklagi umekuwa mali ya wafalme wa Yuda tangu wakati huo. 7 bDaudi akaishi katika nchi ya Wafilisti muda wa mwaka mmoja na miezi minne.

8 cBasi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.)
Copyright information for SwhNEN