‏ 1 Samuel 23:1-2

Daudi Aokoa Keila

1 aDaudi alipoambiwa kuwa, “Tazama, Wafilisti wanapigana dhidi ya Keila nao wanapokonya nafaka katika sakafu za kupuria,” 2 bakauliza kwa Bwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?”

Bwana akamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uuokoe Keila.”

Copyright information for SwhNEN