‏ 1 Corinthians 12:12-14

Mwili Mmoja, Wenye Viungo Vingi

12 aKama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. 13 bKwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

14 cBasi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi.
Copyright information for SwhNEN